Animal Welfare
Research and Data
PUBLIC PROFILE
Wataalamu kuja na mikakati ya kulinda Punda ndani ya Afrika

Added by Patricia Lumba
3 days ago
Linked from: youtube
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wataalamu wa nchi 20 za Umoja wa Afrika ambao wamekutana leo jijini Dar es Salaam kwa mkutano wa siku mbili kutafuta mwarobaini wa kitaalamu wa kudhibiti kasi ya upoteaji wa punda barani Afrika.
Ulega amewataka wataalam kutoka katika nchi hizo kujadili kwa kina na kutoa mapendekezo ya kitafiti na kisayansi kuhusu njia zinazoweza kutumika kuwaokoa wanyama hao na kuziwasilisha ili zijumuishwe katika sera na kanuni kwa ajili ya utekelezaji.
#AzamTVUpdates #MkutanoWaWafugaji #MifugoAfrika #Punda